Serikali ya wanafunzi Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAASO imewapongeza waandaaji wa tamasha kubwa la ugawaji tuzo kwa wanachuo wenye vipaji nchini Tanzania (Silent Ocean Uniawards) linalofanyika IAA kwa mwaka huu. Akizungumza kwa niaba ya rais leo 24 April, 2026 katika semina ya "Kontena la Fursa" , Mhe. Frank Michael ambaye pia ni Waziri wa Habari na Mawasiliano amesema tamasha hilo ni fursa na wanafunzi wa IAA wenye vipaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka washindi wa tuzo hizo. Hata hivyo, leo wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamepata fursa ya kushiriki semina maalum iliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu biashara na utambuzi wa fursa za kujipatia kipato mtandaoni. Kupitia semina hii ya leo April 24, 2026, wanafunzi wamejifunza mbinu tofauti za kuanzisha na kuendesha biashara, pamoja na uelewa wa njia bora za usafirishaji wa bidhaa, huku wakisisitizwa umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kama nyenzo muhimu katika kukuza biashara na kuongeza vipat...