Kikao
maalum cha mapokezi ya mgeni rasmi katika sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa
mwaka wa kwanza kwa mwaka 2026, ndani ya Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA maarufu
IAA WELCOME FRESHERS' PARTY.
Mapokezi
haya yamefanyika katika ukumbi wa PGB tarehe 13 Februari, 2026 usiku, ambapo
mgeni rasmi Mhe Halidi Mwinyi @mwinyi_halid ambaye ni
Katibu Mkuu UVCCM Taifa alipokelewa rasmi.
Katika
kikao hiki Mlezi wa Wanafunzi-IAA Nadhiru Abdulnuru amemkaribisha sana Halid
Mwinyi katika sherehe hizo, na kusema yeye kama kijana ni mfano bora kwa vijana
wa IAA ambao pia wana ndoto za kuwa viongozi wakubwa kitaifa.
Naye
rais wa serikali ya wanafunzi-IAASO Francis Wambura amemshukuru Katibu Mkuu
UVCCM Taifa mhe Halid Mwinyi kwa kukubali mualiko huo wa kuwa mgeni rasmi
katika sherehe hizo za usiku wa tarehe 13 Februari, 2026 katika viwanja vya
michezo IAA.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria kikao na sherehe hizo ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa
Arusha, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha, Diwani wa Kata ya Engutoto,
Marais na makamu wa rais wa vyuo mbalimbali mkoa wa Arusha (Tengeru, TUMA, ATC,
IAA-Kampasi ya Babati nk), Mawaziri, manaibu mawaziri pamoja na makatibu wakuu
wa wizara mbalimbali wa serikali za wanafunzi vyuoni na wageni wengine
waalikwa.







