MAMLAKA ya usimamizi wa Bima (TIRA) kanda ya kaskazini imeandaa Tamasha kubwa la elimu ya bima na michezo katika chuo cha uhasibu Arusha kwa lengo la kujengea uwezo kuhusu maswala ya bima ambapo zaidi ya wanafunzi mia tatu wamehudhuria tamasha hilo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo ndani ya Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA Machi 21, 2026 Meneja wa Bima kanda ya kaskazini
Dokta Emmanuel Lupilya amesema kuwa, kupitia tamasha hilo wanafunzi hao
wameweza kupata elimu kuhusu maswala mbalimbali ya Bima na kuweza kuzijua
faida za kukata bima mbalimbali.
Dkt.
Lupilya amewaasa wanafunzi waliopo vyuo mbalimbali nchini kuhakikisha swala la
bima haliepukiki kwani ndio uti wa mgongo katika kuhakikisha uchumi
unajengwa sio tu kwa fedha bali kwa misingi ya kuwekeza kwenye bima kukinga
mali, afya pamoja na jamii yote kwa ujumla wake.
“jamii
inayofundishwa na kuelimishwa juu ya elimu ya bima hakika serikali yake haiwezi
kubeba mzigo mzito wa majanga hivyo tunahamisha hayo majanga kuelekea kwenye
makampuni ambayo tunayasajili sisi kama mamlaka ili kuona kuwa shughuli zote za
uchumi kijamii zinazoendeshwa na wananchi zinaenda kukingwa na bima .”amesema
Dkt.Lupilya.
Amesema
kuwa ,mamlaka ya Bima ipo kwa ajili ya kukinga ndoto za wadau wote
wakiwemo jamii,wanafunzi ,na ndicho kimewafanya kufika chuoni hapo
kutoa elimu upande wa bima na michezo ili michezo iwaandae vijana hawa kuwa
wabunifu na weledi katika maswala ya kuonesha ukomavu kwenye uongozi kwa
baadaye .
“Tumeanza
leo kwenye chuo cha uhasibu Arusha lakini ndoto zetu ni kufika mikoa na wilaya
zote ambazo tunazisimamia kupitia Kanda hii ya Kaskazin .”amesema .
Aidha
ametaja matarajio yao ya baadaye ni kufikia walengwa zaidi hususani jamii
ambayo haijafikwa na bima na kuweza kufika vijijini na hata maeneo ambayo
wanananchi wanahitaji huduma hiyo ya bima .
“Tumepanga
utaratibu wa kuwafungulia wakala ambao utakuwa ni shirikishi kwa maana ya chuo
wanakuwa na uwakala ili shughuli zote za kusimamia maswala ya kijamii katika
chuo hiki.ziweze kufanikiwa, tutahakikisha makampuni yetu yanatengeza bidhaa
ambazo zinajibu changamoto ambayo imekuwa kubwa katika nchi yetu na kuondokana
na utegemezi kuomba fedha kila wakati na kuona namna ambavyo bima itasaidia
nchi na kusonga mbele na kuhakikisha ndoto za hawa wanafunzi zinafikiwa
.”amesema Dkt.Lupilya.
Massawe
amesema kuwa,wanafunzi zaidi ya Mia tatu wamejitokeza kupata elimu ya maswala
ya bima ambapo kupitia tamasha hilo ambalo limeleta hamasa kubwa sana
wameweza kuwafikia watu wengi zaidi.
“Natoa
wito zaidi kupitia Tamasha hili wanachuo na wananch kwa ujumla
wajue umuhimu wa kukinga mali zao dhid ya majanga kupitia Bima na kulinda afya
zao kwakuwa na bima .”amesema .
Amesema
lengo la kufika chuoni hapa ni utaratibu wao kama Mamlaka kwa ajili ya kutoa
elimu hivyo kundi hili la chuo ni moja ya wadau ambao wanafanya nao kazi kwa
karibu sana na lengo kubwa ni kuwandaa kuwa mabalozi wazuri katika kuwafikia
wananchi kupitia utoaji Elimu ya bima ili kuendeleza SOKO la bima nchini.


