ISRC, BARAZA LA MAWAZIRI WAKUTANA KUJADILI MABADILIKO YA KATIBA

 

Bunge la Wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha-ISRC limekutana Machi 6, 2026 na kujadili mabadiliko ya Katiba ya Serikali ya Wanafunzi-IAASO.


Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa PGB 3, kilihudhuriwa na wabunge wa kampasi zote za IAA kwa njia ya  mtandao (ZOOM MEETING) na kimeongozwa na mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Devis Eugine pamoja na viongozi wengine wa Bunge akiwemo Katibu wa Bunge Mhe. Stephen Mushi.


Kwa upande wa Serikali ya wanafunzi, Waziri Mkuu Mhe. Mollel Mapene pamoja na Baraza zima la mawaziri walihudhuriwa kikao hicho, kilichohusu mabadiliko ya katiba ya serikali ya wanafunzi.


Itakumbukwa kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefika katika kampasi zote za Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA ambazo ni Arusha, Babati, Dar Es Salaam, Dodoma, Songea na Bukombe kuanzia Februri 20, 2026 ili kukusanya maoni ya wanafunzi kuhusu madhaifu na ubora wa katiba iliyopo, na kuwapa nafasi wanafunzi ya kupendekeza mabadiliko gani yawepo.