RAIS WAMBURA ASHIRIKI KWIBUKA 32 [KUMBUKIZI MAUAJI YA KIMBARI RWANDA 1994]

 

HOTUBA

Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Cha Uhasibu Arusha Mhe. Francis Wambura ametoa pole za dhati kwa Jumuiya ya Wanyarwanda, manusura, na wote wanaoendelea kubeba maumivu na kumbukumbu za Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 nchini Rwanda na kusema kumbukumbu, mshikamano, na heshima inapaswa kutunza.


Mhe. Wambura amesema kufikiria kuhusu tukio hilo, ni muhimu ili kuweza kujumuika na kuhakikisha vijana wanakuwepo katika maeneo ya kumbukumbu. Hata hivyo, amesema ukichunguza kwa undani historia ya Rwanda kabla ya 1994, wakati wa Mauaji ya Kimbari, na hata baada yake, inakuwa wazi kwamba nafasi ya vijana si ya ishara tu ni ya msingi kabisa.


However, when we look more closely at the history of Rwanda before 1994, during the genocide against Tutsi, and even in its aftermath, it becomes clear that the role of youth is not symbolic, it is central.


Ikilinganishwa na hali ya sasa ya eneo la Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla, umuhimu wa vijana unaonekana Zaidi, kwani ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pekee, takribani asilimia 65 ya watu wana umri wa chini ya miaka 35. Akiongeza kuwa vijana si kundi dogo la kujumuishwa, wao ndio wengi wanaoamua mwelekeo wa jamii na hivyo si tu kwamba ni sahihi bali ni lazima vijana wazungumze katika nyakati kama hizi si kama nyongeza bali kama wajibu.




VIJANA KUYAFAHAMU HAYA.

Rais wambura ameendelea kusema analizungumzia suala la mauaji si kama Mrwanda, bali kama kijana kutoka katika ukanda wa Afrika Mashariki anayetambua fika kwamba anatoka nje ya historia hiyo na hajapitia uzoefu uliounda yaliyopita ya Rwanda. Lakini kutokana na hilo, vijana wanaweza kukutana na vipengele vya historia hiyo bila kuelewa uzito wake kikamilifu, kwani kuna maneno ambayo hayabebi mara moja uzito wa kihisia.


Maneno yanayotafsiriwa moja kwa moja yanaweza yasionyeshe hatari mara moja. Maneno ambayo awali hayakuwa na maana hasi, bali yalizungumzia umoja. Lakini yalipoingizwa itikadi, yalibadilishwa na hatimaye kuwa kitu tofauti kabisa, jambo ambalo linatoa funzo muhimu kwa vijana wa leo.


This offer an important lesson for us as youth that, what is dangerous is not always obvious at first. Ideas,languages and identities can be gradually reshaped until they become tools of division and harm. We must also confront the difficult truth that a significant number of those who carried out acts of violence during genocide were young people.


Kadhalika, Rais Wambura amebainisha kuwa, mara nyingi vijana sio wapangaji wa mipango, bali husimama katika nafasi ya utekelezaji wa yale yaliyopangwa na kuanzishwa tayari. Katika historia ya vita, mauaji ya kimbari, na migogoro duniani kote, vijana mara nyingi huwekwa mstari wa mbele katika vitendo vya vurugu.


Hata hivyo, ameendelea kuweka wazi kuwa huenda si vijana wote nchini Rwanda walihusika, kwani mara nyingi wapo vijana wanaopinga nia mbaya na vurugu hususani zinapotokea katika nchi. Hata katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994, huenda walikuwepo vijana waliokataa migawanyiko na waliochagua ujasiri badala ya hofu.




MCHANGO WA VIJANA

Rais Wambura amebainisha kuwa inatambulika pia kwamba ukombozi na ujenzi upya wa Rwanda baada ya Mauaji ya Kimbari ulifanywa kwa kiasi kikubwa na vijana, wengi wao waliokulia uhamishoni, wakikabiliwa na changamoto, umaskini, na hasara, lakini wakiwa wameunganishwa na maono ya mustakabali tofauti. Hali inayoonesha kwamba hata katika mazingira yale yale ya maumivu, upungufu na simulizi hatarishi, bado chaguzi tofauti zinawezekana na mara nyingi chaguzi hizo huathiriwa na mawazo na mazingira yanayowazunguka watu.

 

Usahihi wa historia


Rais Wambura amesema vijana wengi waliopo hawakuwa hai mwaka 1994, kwani wengi historia hii si waliyoishi bali wamejifunza. Historia ambayo inapitishwa kupitia familia, simulizi, elimu na kwa kiwango kikubwa zaidi sasa kupitia majukwaa ya kidijitali.


Aidha amesema hali hii imeleta fursa na hatari pia. Kwa upande mmoja, upatikanaji wa taarifa haujawahi kuwa mkubwa, nafuu, na rahisi hivi. Vijana wanaweza kujifunza, kulinganisha mitazamo, kushiriki mijadala, na hata kuhamasisha mabadiliko chanya na kwa upande mwingine, majukwaa ya kidigitali yanaweza kupotosha ukweli kwa kuunda mazingira ya sauti zinazofanana, kukuza ukweli nusu na kuinua sauti zisizo na msingi wa ukweli.



Kwa wale ambao hawakushuhudia historia moja kwa moja, kutofautisha kati ya ukweli na upotoshaji kunazidi kuwa changamoto. Pia mienendo ya kutia wasiwasi duniani, ambapo itikadi hatarishi na alama zake wakati mwingine zinachukuliwa kirahisi, kubadilishwa maana au kuwasilishwa kwa namna inayozifanya zionekane za kawaida au hata kutokukubalika.


Rais Wambura ameweka bayana kuwa kukanusha mauaji ya kimbari, kubadilisha historia na kusambaza simulizi za uongo bado vinaendelea, kwa sababu zamani vilitegemea mifumo ya kati, sasa vinaenea kwa kasi kupitia majukwaa yanayoendeshwa na algoriti, yanayopendelea ushiriki hata kama yanakuza maudhui yenye mgawanyiko na hisia kali.



Je, sisi kama vijana wa kimataifa tunaweza kufanya nini leo?

Rais Wambura amehitimisha kwa kusema vinaja wanaweza kujitolea kulinda ukweli wa kihistoria, kukataa kusambaza simulizi ambazo hazijathibitishwa, kupinga kukanusha na upotoshaji popote vinapoonekana, kuhamasisha umoja katika jamii na kusimama pamoja si tu kwa kumbukumbu bali kwa vitendo.


Hata hivyo, amesisitiza kuchukua kumbukumbu hiyo katika namna watu wanavyofikiri, wanavyosema, na wanavyotenda ili kauli ya “Haitatokea Tena” iwe uhalisia unaojengwa kwa vitendo, si ahadi inayorudiwa tu.