Katika kuimarisha ushirikiano
wa kiuongozi, Waziri Mkuu Mhe. Mollel Mapene pamoja na Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Devis Eugine wamefanya ziara rasmi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar
(ZU) ili kukuza mahusiano kati ya IAASO na Serikali ya wanafunzi ya chuo hicho
(ZANUSO).
Pamoja na mambo mengine,
katika mazungumzo yao na ZANUSO, viongozi hawa wamejadili kuimarisha undugu na
ushirikiano wa kimkakati katika masuala ya kitaaluma, michezo, na uongozi baina
ya serikali zote mbili.
Mhe. Mapene ameeleza ziara hii
kama hatua muhimu katika kujenga umoja wa wanafunzi wa Tanzania Bara na
Visiwani, na kutoa mwaliko rasmi kwa ZANUSO kutembelea IAA ili kuendeleza zaidi
ushirikiano huu.
