Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA
Mhe. Francis Wambura ameipongeza Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za
kulevya kanda ya kasikazini-DCEA pamoja na IAA, kwa kuandaa warsha ya kutoa
elimu ya uhamasishaji wa kuzuia matumizi ya dawa za kulevya na uelewa wa afya
ya akili.
Akizungumza Machi 6, 2026 katika ukumbi wa CH3-IAA wakati akitoa hotuba yake Rais Wambura amesema
maadhimisho ya siku ya wanawake kimataifa ni ishara ya kuikumbusha jamii juu ya
umuhimu wa wanawake katika maendeleo mbalimbali, akisema wanawake ni nguzo
muhimu katika kujenga jamii yenya usawa, maendeleo na ustawi
Aidha, Rais Wambura ameongeza kuwa suala la matumizi ya dawa
za kulevya pamoja na changamoto za afya ya akili ni masuala yanayohitaji
umakini mkubwa, hasa kwa vijana na wamafunzi wote kushirikiana na kuhakikisha
wanajenga mazingira salama yanayofanya watu kuwa na afya njema, nidhamu na
malengo mema.
Kwa niaba ya serikali ya wanafunzi-IAASO Rais Wambura
ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya
Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya-DCEA katika kuelimisha vijana na
kuzuia matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kujenga uelewa wa afya ya akili.
