IAASO YAWAPONGEZA WAANDAAJI TAMASHA LA SILENT OCEAN UNI AWARDS 2026

Serikali ya wanafunzi Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAASO imewapongeza waandaaji wa tamasha kubwa la ugawaji tuzo kwa wanachuo wenye vipaji nchini Tanzania (Silent Ocean Uniawards) linalofanyika IAA kwa mwaka huu.


Akizungumza kwa niaba ya rais leo 24 April, 2026 katika semina ya "Kontena la Fursa", Mhe. Frank Michael ambaye pia ni Waziri wa Habari na Mawasiliano amesema tamasha hilo ni fursa na wanafunzi wa IAA wenye vipaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka washindi wa tuzo hizo.


Hata hivyo, leo wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamepata fursa ya kushiriki semina maalum iliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu biashara na utambuzi wa fursa za kujipatia kipato mtandaoni.


Kupitia semina hii ya leo April 24, 2026, wanafunzi wamejifunza mbinu tofauti za kuanzisha na kuendesha biashara, pamoja na uelewa wa njia bora za usafirishaji wa bidhaa, huku wakisisitizwa umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kama nyenzo muhimu katika kukuza biashara na kuongeza vipato vyao.


“Dunia imekuwa ya kidijitali, na bidhaa nyingi sasa zinapatikana mtandaoni. Vijana wanapaswa kutambua na kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kibiashara,” amesema Mkuu wa Idara ya Masoko kutoka Silent Ocean, Ntwa Kyungu.


Semina hii iliyoandaliwa na SILENT OCEAN UNIAWARDS kwa jina la “Kontena la Fursa,” imefanyika katika ukumbi wa CH3 ndani ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na imeshirikisha wanafunzi wa IAA na wengine kutoka katika vyuo mbalimbali vilivyopo jijini Arusha.


Picha za matukio: