Timu ya mpira wa miguu ya wanafunzi wa Astashahada (Certificate)
IAA imepoteza mchezo wao wa pili dhidi ya timu ya wanafunzi wa Shahada mwaka wa
pili, katika mechi za kusherehekea mapokezi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza IAA
(Freshers’ party matches) kwa kukubali kichapo cha magoli mawili kwa sifuri
(0:2).
Hata hivyo, bado timu hiyo inaendelea kupoteza uwezekano wa
kuwa bingwa wa mashindano hayo ya mpira wa miguu, kwani hapo awali katika
mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu ya shahada (bachelor degree) mwaka wa tatu
Februari 05, 2026 timu ilipokea kipigo cha magoli mawili kwa moja (2:1).
Mbali na mchezo huo, timu ya wanafunzi wa shahada mwaka wa
pili imetoa sare ya magoli mawili dhidi ya timu ya wanafunzi wa Stashahada
(Diploma) mwaka wa pili.

