NITAWATUMIKIA, KUWATETEA NA KUWAPIGANIA KWA MUJIBU WA SHERIA

 

Rais wa Serikali ya Wanafunzi-IAASO Mhe. Francis Wambura amehakikisha kutumikia, kutetea na kupigania maslahi ya wanafunzi kwa mujibu wa katiba ya IAASO kama dira ya uongozi wake.

Ameyasema hayo leo Desemba 4, 2025 wakati wa College Baraza lililofanyika katika ukumbi wa CH3.

Aidha, kwa upande mwingine Rais Wambura amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii, amani, upendo, mshikamano, kuheshimiana na kukataa ubaguzi wa aina yoyite kwani IAA ni sehemu sahihi ya kujenga ndoto, kupata elimu bora na kufikia mafanikio ya kitaaluma.