HAKUNA MBABE MPIRA WA MIGUU IAA-ARUSHA, BABATI

Timu za mpira wa miguu za wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA kampasi ya Babati na Arusha wameshiriki mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu katika viwanja vya michezo kampasi ya Arusha, ikiwa moja ya burudani katika ziara yao waliofanya katika kampasi ya Arusha.

Mchezo huo umechezwa Januari 09, 2026 na timu zote ziliibuka na ushindi wa mabao mawili (2:2), licha ya ushindani mkubwa wa kimchezo uliyoonesha uwanjani na timu hizo.

Awali alipozungumza na kituo cha televisheni cha IAA (IAA Media) rais wa IAA-kampasi ya Babati Mhe. Tyson Mgaya aliahidi ushindi kwa timu yao, akisema wachezaji wao wamejiandaa vya kutosha.