IAA YAZINDUA KLABU YA KUKUZA UPEO WA UONGOZI NA KUJITEGEMEA KWA WANAFUNZI

 

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) leo Desemba 13, 2025 katika ukumbi wa PGB3 kimezindua klabu ya Unite Club ambayo Kaimu Meneja wa Kampasi ya Arusha, Bi. Ester Salahot amesema inalenga kuwawezesha wanafunzi kujitegemea, kuwa viongozi bora na kuchangia maendeleo endelevu ya jamii pamoja na kuleta mabadiliko chanya ndani na nje ya chuo. 

Awali akiwasilisha mada, Mwezeshaji wa Klabu hiyo David Bitaho amesema klabu itatoa udhamini kwa wanafunzi, kukuza vipaji na bunifu, kuimarisha uongozi katika nyanja mbalimbali na kuendesha kampeni za kijamii ikiwemo kuwasaidia watu wasiojiweza na kuhifadhi mazingira kupitia upandaji wa miti.

Makamu wa Rais IAASO Mhe. Ester Emmanuel, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Dennis Rwamkwemba pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo wamesema klabu imekuja kwa wakati muafaka kwani itaongeza thamani ya elimu wanayopata IAA na kuwa chachu ya kuwasaidia kufikia ndoto zao za maisha na maendeleo baada ya masomo.