WANAFUNZI IAA-BABATI WAFANYA ZIARA IAA-ARUSHA

Wanafunzi kutoka Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA kampasi ya Babati wametembelea kampasi kuu ya Arusha, kwa lengo la kushiriki michezo na kujenga urafiki na ushirikiano zaidi na wanafunzi wenzao wa kampasi kuu.

Akizungumza wakati akiwapokea wanafunzi hao, rais wa serikali ya wanafunzi IAASO-Arusha Mhe. Francis Wambura ameipongeza menejimenti ya kampasi ya Babati kwa kuruhusu wanafunzi hao kufanya ziara na kueleza kuwa itasaidia kujenga uhusiano mzuri kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake rais wa serikali za wanafunzi kutoka kampasi ya Babati Mhe. Tyson Mgaya, ameishukuru IAASO-Arusha kwa mapokezi mazuri na kusema ziara hiyo imelenga kuwafanya wanafunzi kufahamiana, kujua mazingira ya kampasi kuu na kujenga urafiki zaidi.

Hata hivyo, katika ziara hiyo wanafunzi wa kampasi zote wameshiriki michezo ya kirafiki ya mpira wa miguu na mpira wa pete katika viwanja vya michezo kampasi ya Arusha.