IAASO YAPOTEZA MCHEZO DHIDI YA TIMU YA WATUMISHI WA CHUO-IAA



Timu ya Serikali ya wanafuzi Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAASO chini ya Rais Wambura imepoteza mchezo wa mpira wa miguu wa ufunguzi wa michezo ya wiki ya sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2025/26 (IAA FRESHERS’ WEEK).


Timu ya Baraza la Mawaziri iliyoungana pia na Wabunge (CRs) imepoteza mchezo huo uliyochezwa leo 05 February, 2026 katika uwanja wa michezo IAA dhidi ya timu ya watumishi wa chuo  kwa kufungwa magoli mawili kwa sifuri (2:0).


Kwa upande mwingine, timu ya wanafunzi wa Shahada wa mwaka wa watatu (Bachelor III) imeibuka mshindi kwa kufunga magoli mawili kwa moja (2:1) katika mechi yao dhidi ya timu ya wanafunzi wa ngazi ya Astashahada (Certificate).