IAA YAIBUKA MSHINDI MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA UDOM

 

Timu ya mpira wa miguu ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) imekubali kupokea kichapo cha magoli 3 kwa 1 katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya wanafunzi kutoka IAA-Arusha.


Akizungumzia kupoteza mechi hiyo, Kapteni wa timu ya UDOM Ally Msabaha amesema mchezo una matokeo matatu kushinda, kufungwa na kupata sale, wao wamekubaliana na kupoteza mchezo. Huku, baadhi ya wachezaji wake wakilalamikia baadhi ya maamuzi ya refa wa mchezo.


Kwa upande wao timu ya IAA, iliyoibuka mshindi wa mechi kwa kupata mabao 3, ikiongozwa na kocha Keba wamesema IAA ina vijana wenye vipaji na mazoezi ya kila siku hivyo, kwa mechi ya muda wowote wapo tayari.