Wanafunzi kutoka IAA waliowakilisha chuo katika shindano la
mabingwa wa mtandao 2025/26, wamemaliza shindano hilo kwa kufikia hatua ya
fainali ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.
Shindano la Cyber Champions lilifikia ukomo Januari 29, 2026 katika
ukumbi wa Papu Tower Arusha, na lililenga kuibua vipaji, kuimarisha uelewa wa
usalama wa mtandao na kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.
Wanafunzi kutoka IAA walioshiriki shindano hilo ni pamoja Michael
Charles, Alvin Mkauzeni, Sadock John, Kasimu Idd, Isaak Simon, William Edward,
Dickson Matiya, Hadi Bakari, Anasi Shabani, Frank Karani, Abel Innocent na
Rodgers Ombeni.
Aidha, walipoeleza faida walizopata katika ushiriki wa shindano
la Cyber Champions 2025/26 wanafunzi wa IAA wamesema imewapa elimu Zaidi kuhusu usalama mtandaoni na
kuongeza kuwa imewajengea uwezo na kujua mambo mengi Zaidi kuhusu mtandao.
Hata hivyo, Shindano la mabingwa wa mtandao (Cyber Champions
Competition 2025/26) lililoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA na
lililowakutanisha washiriki 1,226 waliosajiliwa kutoka vyuo takribani 29 baada
ya hatua za awali na nusu fainali, washiriki 50 bora miongoni mwao kutoka IAA
walifanikiwa kufika hatua ya fainali na Chuo Kikuu cha Dodoma-UDOM kikaibuka mshindi
wa jumla baada ya kutoa washindi wote wanne wa kitaifa.
