BAADA YA KUFUNGWA WABUNGE WATAKA MECHI IRUDIWE

    
Bunge la Wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha-ISRC limelalamika na kutaka mechi iliyochezwa tarehe 23 Januari, 2026 irudiwe kwa wakati mwingine.

Baadhi ya wabunge wameeleza hayo baada ya kumlalamikia muongoza mchezo (REFA) kuwa hakutenda haki baada ya goli lao kukataliwa kwa sababu ya kuonekana kuwa ilikuwa Offside.

Mchezo huo ambao uliohusisha timu mbili (Bunge Vs Baraza la Mawaziri) ulihudhuriwa na viongozi wa juu wa Serikali-IAASO na viongozi wa Bunge akiwemo Spika, umetamatika kwa timu ya Bunge kukubali kichapo cha goli 1.