KLABU YA KUSAIDIA WATU WASIOJIWEZA YATAMBUA MCHANGO WA RAIS WAMBURA


Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAASO Mhe. Francis Wambura amepokea cheti maalum kutoka katika klabu ya Hope for Students Tanzania iliyopo IAA, kama sehemu ya kushukuru na kutambua mchango wake katika safari yao ya kusaidia watu wasiojiweza.

Wakati akiwasilisha cheti hicho leo Januari 15, 2026 Afisa TEHAMA kutoka klabu hiyo Daudi Richard ambaye pia ni mwanafunzi wa IAA, amesema kuwa Mhe. Wambura ametoa mchango mkubwa katika kuwezesha na kufanikisha, tukio lao la kwenda kusaidia watoto yatima waliopo katika kituo cha Momera Center, USA river mkoani Arusha, tukio walilofanya Januari 10, 2026.


  UNAWEZA KUTAZAMA HII