Rais wa Serikali ya Wanafunzi-IAASO Mhe. Francis Wambura amewataka wanafunzi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kuwa mabalozi na kutumia elimu waliyopata kuwaelimisha wengine dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.
Aidha, amepongeza maamuzi yaliyofanywa ya kuichagua IAA kuwa sehemu ya kuadhimisha siku ya UKIMWI dunia katika Wilaya ya Arusha mjini, kwani imewapa wanafunzi fursa ya kujifunza mengi dhidi ya maambukizi hayo.
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika wilaya ya Arusha Mjini yenye kauli mbiu “IMARISHA MWITIKIO TOKOMEZA UKIMWI” yamefanyika leo Disemba 1, 2025 katika ukumbi wa maktaba-IAA na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Arusha mjini, uongozi wa chuo na taasisi binafsi za kupambana na Virusi Vya UKIMWI.
MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
